Habari Kitaifa

RC Makonda Aongeza Muda Zoezi la Usikilizwaji wa Akina Mama

on

Mkuu  wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameongeza muda wa siku tano katika  zoezi la usikilizwaji  wa malalamiko ya akina mama waliotelekezwa watoto huku idadi ya  wananchi waliofika leo ikiwa ni zaidi ya 17,000 na idadi ya wananchi  waliosikilizwa ikiwa ni 7,000  na kupelekea idadi ya watu zaidi 10000  kuwa hawajasikilizwa  bado huku akitoa mapendekezo ya kuunda  kamati ya kupitia sheria ya mtoto.

Akizungumza na akinamama waliofurika ofisini kwake leo, Makonda ameeleza kuwa wanaume walioitikia wito wa kufika ofisini kwake ni 1,500 huku wanaume 1,200 wamekubali kuwatunza watoto kwa kuandikishiana na kueleza kwamba mwanaume yeyote atakayepigiwa  simu au kuletewa barua ya wito na kukaidi kuanzia jumatatu watakamatwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Nitaunda kamati itakayokuwa na wanasheria na watu wa ustawi  wa jamii ili tujue tatizo  ni nini wataalamu wa sheria naustawi wapitie  na mimi ndoto yangu nataka nitengeneze mfumo mzuri  maana uliopo sasa unaonekana umeshindwa kuwasaidia akina mama hawa, na kamati hiyo itakuwa inatoa na kuchambua matatizo ya akina mama” amesema Makonda.

Pia ametoa wito wa kusitishwa zoezi la utoaji namba mpya ili kuendelea kwanza kuwa hudumia wale waliopata namba na hawajapata huduma na kuongeza muda wa siku tano wa usikilizwaji  wa zoezi  hilo na kuongeza “Tunataka katika mkoa huu kina dada wasiwaze kutoa mimba, wasiwaze kutupa kichanga na inaniuma kuona dada amepata mimba alafu anaenda kutupa kichanga, kinondoni kuna kituo cha watoto waliotupwa jalalani na kina watoto 160,”aliongeza Makonda.

Aidha Makonda amesema amesema ifikapo April 25 na 26 atatoa ripoti ya mwelekeo dhidi ya mateso waliyokuwa wakipata kinamama na watoto waliotelekezwa.

Amewataka akina mama kuwa na uvumilivu kwani zoezi hilo limekuwa likibezwa sana na baadhi ya viongozi na kuwataka kutokatishwa tamaa na maneno ya hao viongozi wanayoyatoa kwani hawajui shida na matatizo wanayoyapitia wakina mama hao dhidi  wa  kudai  haki ya watoto wao waliokosa msaada wakati baba zao wapo na wana uwezo wa kuwahudumia watoto.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *