Habari Kitaifa

RC Mghwira Atoa Onyo Kali kwa Wanaoharibu Miundombinu ya Tanesco

on

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira ametoa onyo kali kwa wakazi wa mkoa huo wanaojihusisha na uhabifu wa miundombinu ya Shirka la Umeme Tanzania (Tanesco) na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, serikali inatumia gharama kubwa sana kuendesha shirika hilo hivyo  kulihujumu kwa kuharibu miundimbinu sio sahihi na halivumiliki.

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandisi wa habari, katika kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miumbombinu ya shirika hilo.

“Hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya baadhi ya watu kupoteza maisha baada ya kujaribu kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi na kuwaagiza wakazi wa mkoa huu kuacha kabisa tabia hiyo kwani matukio ya aina hiyo ni sawa na matukio ya uhujumu uchumi, ambayo yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana na hivyo kufikia uchumi wa kati kupita viwanda,” alisema.

Aliongeza kuwa uhujumu wa miundombinu sio tu inaleta hasara kwa shirika lakini pia inapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa kupitia maafa mbalimbali ikiwemo vifo na ulemavu kwa watu wanaohusika na matukio hayo.

Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka alisema changamoto ya  uharibifiu wa miumbombinu unatokana na uelewa mdogo kuhusiana na madhara yatokanayo na umeme.

Pamoja na hayo shirika katika mkoa linajitahidi kufanya uhamasishaji wenye lengo la kuelemisha watu kujiepusha na uharibifu wa miundombinu.

“Tunatoa rai kwa wakazi wa mkoa huu kuwa madhalani wanataka kukata miti ambayo ipo karibu ya  nyaya za Tanesco watoe taarifa ili wataalamu wetu wasaidie kwenye zoezi kwa kinyume na hapo wanaweza kupata matatizo ikiwemo kifo,” alisema Meneja.

Alisema kwa mwaka jana zaidi ya ajali zipatazo 30 ikiwepo ajali za moto na watu kupoteza maisha kutokana na matukio mbalimbali, “Nia ya shirika ni kuona tunamaliza mwaka bila ajali hata moja inayotokana na umeme,”.

Aidha, maneja alisema kwa mwaka mkoa unapoteza asilimia mbili ya mapato yanayotokana na wizi wa umeme na uharibifu wa miundombinu ambapo fedha hizo zingetumika kuboresha zaidi upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Meneja huyo amewaomba wakazi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na shirika ili kuwabahini wanaoendeleza vitenda vya wizi na uharibifu.

Alisema mwaka jana pekee zaidi ya Sh50 milioni zilipatikana kutoka na faini mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa miundombinu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *