Viwanjani

SDA Yakabidhi Vifaa vya Michezo Mtwara

on

Shirika la msaada wa  maendeleao ya Michezo SDA mkoa wa Mtwara limefanikiwa kutoa mafunzo pamoja na vifaa vya michezo kwa shule mbili za msingi libobe pamoja na sekondari zilizopo kijiji cha Libobe kilichopo wilaya na mkoa wa Mtwara.

Mafunzo hayo yamelenga Kujenga uwezo kwa wanafunzi hasa wa kike katika maswala ya Afya Kupitia Michezo pamoja na kujua haki zao ili kuweza kujiamini katika kutoa maamuzi mbalimbali ya maisha yao.

Meneja Mradi wa Mradi wa Kuwezesha wasichana Kupaza sauti  Unaoendeshwa na SDA Thea Swai  amesema Mradi huo unaendeshwa katika kata Tisa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara manispaa kwa lengo la kuelimisha na kujengea Uwezo wa Umuhimu wa Umuhim wa Elim kwa wasichana na Jamii kwa ujumla .

“Lengo kuu la Mradi huu ni kuelimisha na Kujengea Wasichana na Jamii kuhusu Umuhim wa Elimu kwa ujumla juu ya upatikanaji Ushiriki na ufikiwaji wa elim ya msingi na sekondari hasa kwa watoto wakike ambao wamekuwa wahanga wa matatizo ya ufaulu mdogo wanapomaliza elim ya sekondari na wakati mwingine kwa idadi ndogo ya wasichana wanaomaliza shule za sekondari,”.

Lakini naye Afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Mtwara vijijini Maisha Mlaponi amewaomba wazazi kuhakikisha wanawajengea Uwezo wa Kujiamini wanafunzi ili waweze kufanya Vizuri wawapo darasani.

“Wazazi naombeni Muwasaidie watoto wenu wa Kike waweze kujiamini katika Maisha yao na wakiweza kujiamini hata darasani wataweza kufanya vizuri  kwa sababu watakuwa na uwezo wa kuuliza maswali kwa walim na hivyo wataweza kuelewa na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho,”.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *