Habari Kitaifa

Serikali Yadhamiria Kumlinda Mtoto Dhidi ya Ukatili Mtandaoni

on

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamilia kumlinda mtoto dhidi ya ukatili ukiwemo unyanyasaji wa mtandaoni.

Katika kulifanikisha hilo Wizara imekutana na wadau wa maendeleo ya Mtoto Jijini Dodoma kujadili kuhusu namna bora ya kupambana na ukatili wa mtoto mtandaoni ambao unaenea kwa kasi kubwa na kutishia usalama wa mtoto na jamii kwa ujumla.

Akifungua kikao kati ya Serikali na wadau wa Maendeleo ya Mtoto, Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba amesema kuwa Serikali haitafumbia macho matumizi ya mitandao ambayo yana athari mbaya kwa mtoto na watahakikisha kunakuwa na udhibiti wa matumizi ya mitandao ili kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono mtandaoni.

Bw. Marcel Katemba ameleza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau katika mapambano dhidi ya ukatili wa kingono kwa mtoto mitandaoni, hivyo kwa pamoja watashirikiana kuhakikisha kuwa vita ya kupambana na ukatili dhidi ya Mtoto ikiwemo ukatili wa mtandaoni inafanikiwa.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau katika ulinzi na usalama wa mtoto na Serikali itaendelea kushirikiana na wadau ili kupata mbinu na namna sahihi za kupambana na ukatili ili kulinda mtoto  dhidi ya madhara ya matumizi maovu ya mitandao.

Katemba amesisitiza kuwa suala la ukatili wa mtoto lina madhara makubwa kwa mtoto na jamii ya Kitanzania hivyo jitihada za pamoja zinahitajika kushirikiana na wadau wa maendeleo ya mtoto kupambana na ukatili huo.

“Sisi tupo tayari kupambana na ukatili wa mtoto mtandaoni na tutalisimamia hilo ili tuondokane na ukatili huu” alisisitiza Bw. Katemba

Kwa upande wake  Mhadhili wa Chuo cha Ualimu Dar es salaam (DUCE) Dkt. Hezron Onditi akiwasilisha utafiti kuhusu hali ya ukatili wa mtoto mtandaoni, amesema kuwa tatizo la ukatili wa mtandaoni kwa mtoto ni kubwa na linaenea kwa kasi na mpaka sasa takribani asilimia ya 5 – 72 ya watoto na vijana wadogo duniani wamefanyiwa ukatili wa kingono mtandaoni ikilinganishwa na asilimia 58 ya watoto waliofanyiwa ukatili huo kupitia matumizi ya simu na mitandao hapa nchini.

Dkt. Onditi ameongeza kuwa tatizo la ukatili wa kingono kwa njia ya mtandao ni changamoto kubwa maana unyanyasaji huo kwa kiasi kikubwa hufanywa na watu wenye mahusiano ya karibu wakiwemo marafiki, kundi rika, na watu wasiojulikana.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto Bi. Magreth Mussai amesisitiza a kuwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia na kuimarisha malezi ya mtoto katika mazingira ya shule na majumbani ili kuzuia athari mbaya zinazosababishwa na matumizi mabovu ya simu na mitandao katika dunia ya teknolojia na utandawazi.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *