Habari Kitaifa

Shirika la Reli Latiliana Saini Makubaliano Ununuzi wa Vichwa 11 vya Treni

on

Shirika la Reli Nchini TRC limetiliana saini ya makubaliano ya kuvinunua Vichwa 11 vya Treni kutoka Kampuni ya Progress Rail Locomotives ya Marekani ambayo inavimiliki Vichwa hivyo Vyenye namba 9014 hadi 9024.

Mnamo Tarehe 27 September 2017 , Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili ya kubaini kama Vichwa hivyo ni vipya au laa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini Bw. Masanja Kadogosa amekutana na Vyombo vya habari, na kutoa taarifa hiyo.

Bw. Masanja amesema kuwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa ya kuvinunua Vichwa hivyo kwa Bei ya Dola za Kimarekani Milioni mbili  na laki nne, badala ya Dola Milioni tatu na laki mbili ambazo zilitumika kununua vichwa 13 mwaka 2015, Serikali imeokoa Dola Milioni nane na laki nane.

Kwa upande  wake Meneja wa Kanda  ya Kusini Mwa Jagwa la Sahara wa Kampuni hiyo ya Progress Rail  Barend Hanekom amesema amefurahishwa kwa  mara nyingine tena kufanya baishara na Serikali ya Tanzania.

Katika Mkataba huo, imelezwa kuwa itapaswa kufanyika kwa majaribio ya Vichwa hivyo kwa awamu tatu, kwanza ni ukaguzi wa kuvitizama , yaani Visual Inspection, pili ni kuviwasha na kuvipa mzigo lakini vikiwa havitembei yaani Load Box, na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo  wenye tani 700 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kasha Tani 1200 kutoka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.

Ununuzi wa Vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa Shirika la Reli kwani sasa hivi Shirika lina Vichwa 29 madhubuti kati ya 47 vinavyohitajika ili kutoa huduma nzuri na uhakika.

 

 

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *