Viwanjani

SIMBA yaunda Kamati ya Usimamizi wa Mauzo ya Hisa za Klabu

on

Klabu ya Simba leo imetangaza majina matano ya wajumbe wanaounda kamati ya usimamizi wa uuzwaji wa hisa za Klabu hiyo yenye makao yake Makuu mitaaya msimbazi jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo mkuu wa idara ya mawasiliano wa Klabu hiyo Haji Manara amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kupitishwa kwa makubaliano ya mabadiliko katika uendeshwaji wa Klabu hiyo.

Kamati hiyo inatarajia kufanya kikao chake cha kwanza tarehe 6 au 7 mwezi huu kikao kitakachokuwa cha kwanza kwa kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Thomas Mihayo.

Akitaja majina hayo Katibu wa Simba Sports Club Dkt Kashembe amemtaja Jaji Thomas Mihayo Mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Mussa Azan Zungu Mbunge wa Ilala, Wakili Damas Ndumbaro, Abdulrazack Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Mtaalamu wa manunuzi Yusuph Nssoro.

Mbali na kutangazwa kwa kamati hiyo pia Simba imetoa onyo kali kwa wanaouza jezi feki kutokana na wao kupata hasara katika wimbi la uuzwaji wa jezi feki huku watu hao wakishusha uchumi wa timu hiyo.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *