Habari Kitaifa

Soma Hii Hapa “Madereva Wazembe na Wakorofi Kula Viboko”

on

 

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), akifafanua jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi  Hamad Massauni.

…………………………………….

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kupitia Jeshi la Polisi inakusudia Kuanzisha Adhabu Kali ya Kuwacharaza Viboko Madereva wa Vyombo Moto Ikiwemo Magari, Bajaj na Pikipiki Watakaobainika Kukiuka Kwa makusudi Sheria za Usalama Barabarani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi HAMAD MASAUNI ametoa Kauli hiyo Mjini Dodoma Wakati akielezea Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani Kwa Kiwango cha Asilimia 10.

Amesema adhabu ya Viboko kwa Madereva Wakorofi na Wazembe amesema itaanza Kutekelezwa Kwenye Awamu ya Pili ya Mkakati huo iliyopangwa Kuanza Mwezi Ujao.

Mhandisi MASAUNI ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa Usalama Barabarani amesema Miezi Sita ya Utekelezaji wa Mkakati huo imekuwa na Mafanikio Baada Kiwango cha Ajali kuonekana Kupungua.

Kwa Upande Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi EDWIN NGONYANI amesema Mfumo wa Pointi Kwenye Leseni ya Udereva ulioanzishwa na Serikali Utasaidia Kwenye Mkakati wa Kupunguza Ajali Nchini.

Kulingana na Tathmini hiyo Kiasi ya Madereva  1596 walikutwa na Hatia ya Kutoheshimu Sheria za Usalama Barabarani, ambapo Walikamatwa na Kupelekwa Mahakamani.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *