Habari Kitaifa

Spika Ndugai awataka Viongozi wa Dini na Watanzania kudumisha Amani na Utulivu

on

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na maendeleo.

Ndugai ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Spika Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka jamii kuendelea kupiga vita uhalifu na kuwafichua wahalifu popote walipo ili nchi iendelee kuwa na amani.

Mratibu na Muandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ni kuwajengea vijana maadili mema ili waweze kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya taifa.

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shabaan amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi qoran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *