Burudani

Tanzania Bara na Visiwani wapendezesha Tamasha la JAMAFEST

on

Wakati tukiwa katika msiu wa Tigo Fiesta 2017 tukiwa tunashuhudia mitambo kibao ilivyowashwa na mpaka kukinukisha huko Mkoani Arusha, Nchini Uganda napo kuna Tamasha la Wajasiriamali linaloendelea kwa sasa linalowakutanisha Wajasiriamali kutoka Nchi zote za Afrika Mashariki zikiwemo, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Baada ya Makubaliano yaliyoafikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ya wanajumuiya wote kuwa kitu kimoja, kulianzishwa Tamasha la Wajasiriamali ambalo linaitwa JAMAFEST (JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI UTAMADUNI FESTIVAL) likiwa na lengo la kuwakutanisha wanajumuiya wote kutooka Nchi za Afrika Mashsriki katika maswala ya Utamaduni, Sanaa na Maonyesho.

Akizungumza na Ramadhani Ismail wa Choice in the Morning, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Eliabi Chadota, anasema kwamba JAMAFEST ni makubaliano ambayo yamefikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha wanajumuiya hiyo kuwa kitu kimoja, marafiki na kikubwa zaidi ni kuweza kufundisha lugha amabazo wanazitumia wanajumuiya ya Afrika Mashariki.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *