Habari Kitaifa

TRA Kuchunguza Ulipaji Kodi wa Askofu Kakobe

on

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema itachunguza mwenendo wa ulipaji kodi wa Askofu Mkuu wa kanisa la FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP ZAKARIA KAKOBE siku chache tu baada ya ASKOFU huyo kutangaza kuwa ana pesa nyingi kuizidi Serikali.

ilikuwa ni kauli ya Kiongozi wa Kanisa la FULL GOSPEL BIBLIE FELLOWSHIP ZAKARIA KAKOBE juu ya fedha alizonazo ambazo zinaizidi Serikiali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tamko hilo ambalo amelitoa siku kadhaa zilizopita limeiamsha mamlaka ya mapato Tanzania TRA ambayo inasema imelipokea tamko hilo kwa mikono miwili.

Katika hatua nyingine Kamishna KICHERE amekiri kuwa Mamlaka hiyo haina taarifa za ulipaji kodi wa Askofu huyo licha ya utajiri Mkubwa alioutangaza.

Timu ya Mamlaka hiyo inatarajiwa kumtembelea ASKOFU huyo muda wowote kuanzia sasa na hapa Kamishna KICHERE anamtaka kuitoa ushirikiano.

 

 

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *