Habari Kitaifa

TRA yazifungia Hotel tatu, Kituo cha Mafuta mkoani MTWARA

on

Mamlaka ya mapato mkoani Mtwara (TRA) imezifungia hotel tatu mkoani humo pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa kodi ya malimbukizo ya madeni.
Hotel zilizofungiwa ni Naff Beach, Naf blue, BNN pamoja na kituo cha Mnarani Petrol Station ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya Sh 1 bilioni ambazo ni malimbukizo ya madeni ya nyuma kwa kipindi cha miaka mitatu.
Afisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.
“Ni madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma,kikubwa walipe kodi..tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbukizo ya madeni ya muda mrefu,matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii sharia za kodi kama kutunza kumbukumbu,”amesema Byabato
Byabato amesema endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao watachukua hatua nyigine kama kukamata mali au kuwapeleka mahakamani kama hawatajitokeza kuomba na kuahidi ni lni watalipa madeni kwani hakuna aliyejitokeza kufanya hivyo.
Aidha amesema pia yapo maduka madogo ambayo yamefungiwa na kwa sasa wako wilayani Masasi wanaendelea na ukaguzi.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *