Habari Kitaifa

TWAWEZA: Bakhshishi kwa Walimu zimeleta Matokeo mazuri

on

Baada ya miaka miwili ya majaribio, Twaweza  kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), pamoja na Shirika la Innovations for Poverty Action (IPA), wameridhihirisha kuwa kuwalipa walimu fedha baada ya matokeo ya kujifunza kunaweza kuboresha matokeo ya kujifunza.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze wakati akitoa Matokeo ya utafiti KiuFunza (Kiu ya Kujifunza) wa awamu ya pili jijini Dar es salaam na kueleza matokeo hayo yamethibitisha kwamba wanafunzi wameweza kujifunza na kupata stadi stahiki kwa muda wa mwaka mmoja kile ambacho wangeweza kujifunza kwa mwaka na nusu muhula.

“Twaweza kwa kushirikiana na IPA tumeonyesha kuwa utoaji wa motisha kwa mwalimu unaweza kuboresha matokeo ya kujifunza japokuwa kujifunza kunachangiwa na mambo mengi tumeonesha kupitia utafiti wa kisanyansi, kuwa kuchanganya motisha na uwajibikaji kunaweza kuleta matokeo mazuri ya kujifunza kwa watoto tuna ushahidi thabiti wa kile kinachoweza kufanyikana kuwa na uhakika kuwa tukifanya hicho watoto watajifunza.” alisema Bw. Eyakuze.

Changamoto kubwa ni namna ya kuwafikia watoto wengi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kufanya mpango huu kudumu kwa muda mrefu kutokana na Serikali ya awamu ya tano kujikita katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa kawaida, tuna imani kuwa utafiti huu utapokelewa na matokeo yake kukubalika katika ngazi za juu za Serikali. aliongeza Bw. Eyakuze

Aidha Bw. Eyakuze aliongeza kuwa matokeo ya utafiti uliojulikana kama KiuFunza utafiti mkubwa wa aina yake Afrika Mashariki, yaliwashilishwa katika majadiliano na  wadau wa elimu jijini Dar es salaam na kwa kipindi cha miaka miwili ya KiuFunza, Twaweza na IPA wamefanya majaribio katika shule 200 kwenye wilaya 21 za Tanzania

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *