Habari Kitaifa

URA Saccos watoa msaada wa vifaa tiba kwa Jeshi la Polisi

on

Jeshi la Polisi Nchini limepokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Usalama wa Rai Saccos (URA Saccos) ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii inayowazunguka huku vifaa tiba hivyo vikitarajiwa kupekekwa kwenye zahanati na Hospital za Jeshi hilo la Polisi zipatazo tisa.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Hospital Kuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Jeshi la Polisi Operesheni na Mafunzo DCP  Nsato Malijani ameishukuru Saccos hiyo ya Polisi kwa kurudisha sehemu ya faida yake katika jamii inayowazunguka na kueleza kila siku huduma hizo zilizokuwa zikikwamishwa na vifaa vichache vilivyokuwapo hapo hivyo kupokea kwa vifaa hivyo  vitasaidia kuongeza huduma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa URA Saccos DCP Azizi Mohamed ameeleza kuwa Saccos hiyo ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na lengo la kuweka na kukopa na wakati inaanzishwa ilikuwa na wanachama 4300 na mpaka sasa ina mtaji mkubwa wa wanachama, hivyo wameamua kutoa msaada wa afya kwa jamii kwani zahanati hizo wanazopeleka vifaa tiba hivyo nao huenda kutibiwa.

“Vifaa  hivi tunaamini vitatusaidia hata sisi askari wenyewe kwani tunaamini wengi wetu tuna hudumiwa na hizi hospitali zetu na napenda kuwasihi kuvitunza ili viendelee kuhudumia kwa muda mrefu na tunaahidi kuendelea kutoa tena msaada wa vifaa vitakavyo hitajika tena”  alisema DCP Azizi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya SACP Paul Kasabago ameishukuru URA Saccos kwa kuwasaidia vifaa hivyo na kuahidi vitatumika kama ilivyokusudiwa.

Vifaa tiba hivyo vilivyotolewa ni vitanda vya kulaza wagonjwa, utrla sound, mawodini na  maabara na vikiwa na thamani ya silingi milioni 100 na vitasambazwa katika zahanati mbalimbali za Jeshi la Polisi Nchini.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *