Habari Kitaifa

Wananchi DSM Waongezewa Siku Usikilizwaji wa Msaada wa Kisheria

on

Kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  ameongeza siku  ya kesho ya jumamosi kuhakikisha wananchi wote waliofika hapo  wanasikilizwa na kuhudumiwa.

Akizungumza na wananchi leo, Mwanasheria wa ofisi ya mkoa wa Dar es salaam Bi. Fabiola Mwingira amesema kutoka na wananchi kuwa wengi tofauti na matarajio, Mhe. Makonda ameamua kuongeza siku moja hadi kesho jumamosi ili wananchi wote waweze kupata  huduma.

Aidha Bi. Mwingira ameeleza kuwa mpaka sasa wameshasikiliza na kuhudumia zaidi ya wananchi 3000 na hivyo kwa kuongeza siku moja hiyo matarajio yao ni kuwa hadi kufikia kesho watamaliza wananchi wote.

Pia amesema baada ya zoezi hilo kumalizika Mhe. Makonda atazungumza na wananchi wote katika  ukumbi wa diamond jubilee siku ya jumamosi tarehe 10 februari  kuanzia saa moja asubuhi ili kuwapa mrejesho wananchi wale wote waliokwisha sikilizwa malalamiko yao.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *