Habari Kitaifa

Wananchi wa LUMWAGO, Mufindi Wapata Umeme Kwa Mara ya Kwanza

on

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha umeme kwa mara ya kwanza katika Kata ya Upendo mtaa wa Lumwago uliyopo wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa. 

Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya mamia ya wananchi wa mtaa wa Lumwago ambao walikuwa na furaha baada ya kuona umeme huo umewaka kwa mara ya kwanza.

Waziri Kalemani alifanya uzinduzi huo akiwa katika ziara ya kazi mkoani Iringa wakati wa kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na REA awamu ya tatu.

Awali, akiongea na wananchi Dkt. Kalemani alisema kuwa wananchi zaidi ya 200 wataanza kupata umeme kufuatia tukio la kurasimishwa kuwashwa kwa nishati hiyo Lumwago. 

“Tunatoa kipaumbele chetu kwa sasa kwani ni kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata umeme na huduma hiyo inakuwa ya uhakika,” alisema Dkt. Kalemani.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi wakishangilia baada ya kuona kweli umeme umewaka katika kijiji cha Lumwago.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa Kwenye furaha ya ajabu baada ya kuona wananchi wake wamefanikiwa kupata umeme katika eneo hilo. 
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiongea mbele ya wapiga kura wake wa jimbo hilo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwaonyesha wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini kifaa cha Umeme Tayari (UMETA).
 
 

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *