Habari Kitaifa

Watoa Huduma za Afya Morogoro wajipanga kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto

on

Watoa huduma wa afya wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepukan na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ili kuhakikisha takwimu za vifo vya akina mama wajawazito haziongezeki kama ilivyo sasa  kwani takwimu zinaonyesha vifo vya akina mama vimeongezaka kutoka 454 katika vizazi hai laki moja  kwa mwaka jana  hadi kufikia vifo 556 kwenye vizazi hai laki moja.  

Rai hiyo imetolewa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk, Frank Jacob katika mkutano wa kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya  kutoka Zahanati na Vituo vya Afya 20 Mkoani Morogoro  ambapo amesema ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito  nilazima wataalamu wa Afya wafate vigezo vya utoaji wa huduma bora kama kuangalia madhurio ya akima mama Clinic, kutoa dozi ya pili (ASP) ya kukinga Maralia , Madini ya chuma na Folic Acid kwa mjamzito  pamoja na kutoa elimu kuhusu uzazi wa mpango ambao pia hupunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 44.

Mafunzo hayo ambayo yanatoa nafasi kwa watoa huduma kutoka katika Zahanati na Vituo vya Afya kuweza kutoa huduma za dharula kwa mama mjamzito na mtoto wamebaisha changamoto mbalimbali ikiwemo ya jinsi ya kutoa huduma kwa mama wenye vifafa vya mimba na wale ambao wanatokwa damu nyingi baada ya kujifungua huku tatizo la usafiri vijiji nalo limeonekana kuwa sehemu ya changamoto.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *