Habari Kitaifa

Waziri Mhagama Kuzifutia Usajili Kampuni Tisa za Wakala wa Huduma za Ajira Nchini

on

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Kamishina Mkuu wa Kazi nchini kuzifutia usajili kampuni tisa za wakala binafsi wa ajira kwa kosa la kubadili anwani za ofisi zao bila kutoa taarifa kwa Kamishina wa kazi na kuto kuwasilisha taarifa kwa kamishina wa kazi mara baada ya mikataba ya kazi ya wafanya hao kukamili.

Aidha Mhe. Mhagama amemuagiza Kamishina wa kazi kuzifanyia uhakiki wakala zote zinazoendesha shughuli za wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini ili kuona kama wanatekereza na kuzingatia matakwa ya sheria ya huduma ya ajira namba 9 ya mwaka 1999 na kanuzi zake kupitia tangazo la serikali namba 232 ya mwaka 2014.

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amechukua uamuzi huo mara baada ya kubaini uwepo wa udanganyigu mkubwa wa  mawakala  na kuelekeza shughuli hiyo ifanywe na wakala wa huduma za huduma za ajira wa serikali katika kipindi hiki cha mpito wakati serikali ikiendelea na jitihada za kuangali namna ya kuingia mikataba na nchi husiska ili kuwa na uhakika na watanzania wanaokwenda kufanya kazi nnje ya nchi.

Aidha waziri mhagama ametuamia nafasi hiyo kuwataka wale wote ambao walikuwa wmesajiliwa na kampuni hizo kwaajili ya kwenda kufanya kazi nnje ya nchi kutoa taarifa haraka kwenye mamalaka hususika ili waweze kupewa malekezo na utaratibu mwingine unaostahili.

Kadhalika Waziri Mhagama amemuelekeza Kamishina wa kazi nchini kuendelea kufuatilia ukweli wa watanzania  elfu 4,118 waliounganishwa na fursa za ajira nje ya nchi ili kujua mahali walipo, mikataba yao na hasa ustawi wa wasichana elfu 3706 walioajiriwa nje ya nchi.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *