Habari Kitaifa

Waziri Mkuchika Ateta na Balozi wa Uswiss

on

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika ameishukuru Serikali ya Uswiss kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwamo masuala ya utawala bora.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Mhe. Florence Tinguely Mattli kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Uswiss imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania katika masuala ya utawala bora ambayo wafadhili wengi hawayapi kipaumbele.

Amezitaja nchi nyingine zinazoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya utawala bora kuwa ni Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la DfID na Marekani kupitia Shirika lake la Misaada la USAID.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wake, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inahakikisha suala la utawala bora linazingatiwa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Kwa upande wake, Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Mhe. Florence Tinguely Mattli ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada wanazozifanya katika utekelezaji wa masuala ya utawala bora na ameahidi kuendeleza ushirikiano.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *