Viwanjani

Waziri Mwakyembe Akutana na Wajumbe wa Bodi ya Filamu na Kutembelea Studio

on

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo (kulia) akitoa taarifa fupi ya majukumu ya bodi ya filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo na wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Filamu (hawapo pichani) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe hao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo

Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Filamu na wajumbe wa kamati ya maudhui ya filamu wakifuatilia maagizo ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *