Habari Kitaifa

Waziri Tizeba aagizwa Kurudiwa Uchaguzi wa Viongozi wa Ushirika penye Dosari

on

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Afisa ushirika wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Gurisha Msemo kufanya ziara ya kikazi maeneo yote kuliko fanyika uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika ili kubaini uhalali wa uwepo wao.

Mhe. Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya wakazi wa Kijiji cha Mkunguakihendo na Misughaa Wilayani Ikungi kuonyesha kutotambua namna walivyochaguliwa viongozi waliopo madarakani kukiongoza chama hicho katika ngazi mbalimbali jambo ambalo lina ashiria kupatikana kwa viongozi hao kinyume na utaratibu.

Dkt. Tizeba ameyasema hayo jana 8 Juni 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida.

“Pamoja na maelekezo yangu ya kutazamwa mahali penye matatizo na kufanyika upya uchaguzi lakini pia nawasihi pindi utakapofanyika uchaguzi mchague viongozi waadilifu ambao watawasimamia katika kweli na haki”

“Kwa muda mrefu sana kwenye vyama vya ushirika karibu nchi nzima watu walikuwa wanagawana vyeo badala ya kuchagua viongozi bora kwa maslahi ya wananchi, lakini katika kipindi hiki tumedhamiria kwa dhati kabisa kuwa na haki katika upatikanaji wa viongozi wa chama chenu,” alikaririwa Mhe Tizeba

Sambamba na agizo hilo pia amewasihi viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika kote nchini kutojihusisha na wizi wa fedha za wananchi kwani kufanya hivyo sio kosa la wizi pekee bali ni kosa la uhujumu uchumi.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu  amewasihi maafisa ugani kuongeza ufanisi katika usimamizi kwenye kilimo ili kuongeza tija itakayopelekea kuwa na mavuno mazuri yenye manufaa makubwa kwa wakulima.

Aliwaomba wataalamu wa utafiti kote nchini kupitia upya katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini dawa bora za kuua wadudu wanaoathiri mazao mbalimbali likiwemo zao la pamba.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *