Uchumi Zone

Waziri TIZEBA ateta na GRAZIANO DA SILVA, Mkurugenzi Mkuu wa FAO

on

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, amefanya mazungumzo na waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi nchini Tanzania. 
 
Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa
Serikali, wadau na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.
 
Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inajili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza
shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 
 
Katika mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Mkuu wa FAO anabadilishana
mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana
na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa
na kikanda.
 
Pia yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala ya umuhimu kati ya pande hizo mbili.
Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa
nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za
utafiti. 

 

Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni
Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba.
Wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kushoto) akiteta jambo na mwenyeji wake Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba mara baada ya kutembelea ofisini kwake. 
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva 
kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *