Habari Kitaifa

Waziri Ummy Kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Rukwa

on

Waziri wa  Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu atashiriki Maadhimishoya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Machi 08 ya kila mwaka kwa kujumuika na wanawake, wadau na wananchi wa mkoa wa Rukwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Sumbawanga.

Bw. Mbilinyi amesema kuwa maadhimisho hayo yalianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani mnamo mwaka 1911 na kuazimiwa kuwa siku rasmi ya Wanawake Duniani katika kikao cha Baraza la Umoja wa Mataifa cha mwaka 1945.

Ameongeza kuwa lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutathmini utekelezaji wa afua za kufikia usawa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi, kijamii, kisiasa katika kufikia maendeleo jumuishi. Maadhimisho haya pia yanatoa fursa ya kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na jamii, Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kumwinua mwanamke wa kitanzania.

 

Aidha, katika kuadhimisha Siku hii wadau wanapata fursa ya kutafakari na kubainisha upungufu uliojitokeza katika utekelezaji na kuzitafuta majawabu ya changamoto zilizobainishwa.

 

Katika muktadha wa Tanzania, Kaulimbiu ya mwaka 2018 ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini.” Kaulimbiu hii inaendana na nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania ya Viwanda na uchumi jumuishi alisema Bw. Mbilinyi. 

 

 Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Rukwa Bi. Aziza Kalyatila  amesema kuwa Mkoa umejipanga kuiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa Jukwaa la Uwezehsaji Kiuchumi la Mkoa na kutoa mitaji kwa wanawake wajasiriamali.

 

Bi Aziza  ameongeza kuwa wamesisitiza Halmashauri kuadhimisha Siku ya wanawake mpaka hadi ngazi ya vijijini ambapo wahusika wakuu wanapatikana huko na pia Kauli mbiu kwa mwaka huu inasisitiza kuwawezesha wanawake hao.

 

Siku ya Wanawake Duniani 2018 kilele chake kitakuwa siku ya tarehe 8 Machi, 2018 na  Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni ‘‘KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI” Dhamira ya Wizara nikuona kila mdau mmoja mmoja anelewa madhumuni ya kaulimbiu na kuchukua hatua kuchangiautekelezaji wa ujmbe wa mwaka huu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *