Habari Kitaifa

Wivu wa Mapenzi: amuua Mume wake kwa Kuichoma Moto Nyumba

on

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Linamtafuta Zuhura Ismail Mkazi wa Halmashauri ya Nanyamba Mkoani Mtwara kwa Kosa la Kumuua Aliyekuwa Mume wake kwa Kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishii kwa kutumia mafuta ya Petrol kutokana na Wivu wa kimapenzi.
Zuhura ambaye anatafutwa na jeshi la Polisi,Majira ya Usiku alifika Nyumbani kwa mume wake huyo ambaye walikuwa wametengana na Kuhisi kuwa Ndani ya nyumba Mumewe alikuwa amelala na mwanamke Mwingine Hivyo Kuchoma Nyumba Moto na Kutokomea Kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amewaomba wananchii wanamfahamu kutoa taarifa popote watakapomuoa Mwanamke Huyo Zuhura Ismail.
Aidha kamanda Mkondya ameongeza kuwa Watu 12 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za Wizi wa pikipiki pamoja na Kuvunja nyumba za watu na kuiba Vifaa mbalimbali vya majumbani.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Limewataka wananchii waliotoa taarifa za kuibiwa wafike kituo cha Polisi kwa ajili ya Kutambua  na kuchukua mali zao.
Pichani.Kamanda Wa Police Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya akiwaonesha waandishi wa Habari Samani za Ndani Zilizokamatwa baada ya Kufanya Opereshen ya Msako kwa Watuhumiwa wa wizi pamoja na Madumu ya Pombe haramu ya Gongo Lita 369 ambapo watu 15 wamekamatwa wakifanya Biashara ya Kuuza na Kusafirisha.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *