Habari Kitaifa

Wizara ya Afya yapokea Bilion 227.76 kusaidia Sekta ya Afya

on

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea shilingi Bilioni 227.76 kutoka kwenye mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwaajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya Afya Nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea fedha hizo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa huduma za Afya Nchini.

“Fedha hizi zitasaidia pia kutoa huduma za chanjo kwani kwani ni hatua muhimu kwa wananchi hususani katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano Nchini” Alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kupeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka changamoto za vituo hivyo kukosa dawa muhimu mara kwa mara.

Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya alisema asilimia 90 ya fedha hizo zinaenda moja kwa moja kwenye vituo vinavyotolea huduma za afya vya ngazi ya Halmashauri na asilimia 10 inatumika kwaajili ya shughuli mbalimbali za usimamizi wa kisera katika sekt ya afya Nchini.

Pia Dkt. Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitasaidia katika kuimarisha miundombinu katika vituo vya afya na zahanati ili viweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwaajili ya akina mama wajawazito wanaokabiliwa na uzazi pingamizi.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark Nchini Tanzania Bw. Einar Jensen kwa niaba ya wadau wa mfuko huo amesema kuwa mbali na Fedha hizo kushughulikia maswala ya afya nchini hapa pia zitakuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo.

” Mbali na kushughulikia masuala ya afya pia napendekeza fedha hizi zihusike katika kuhudumia wakimbizi wanaoingia Tanzania hasa katika maeneo ya Kigoma na Kibondo” Alisema Bw. Jensen.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *